Zoezi la kuchezesha droo hiyo ya Kopa na Bayport likiendelea. Washindi wanne walijishindia Sh Milioni 1,000,000 kila mmoja.
Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo
kushoto, akizungumza jambo kwenye heka heka ya droo ya kutafutwa
washindi wanne wa shindano la Kopa na Bayport linaloendeshwa na Taasisi
hiyo. Aliyefungwa kitambaa usoni ni Meneja wa Bayport Financial
Services, Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Kulia ni Msimamizi wa Michezo
ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo. Washindi hao wanne kila mmoja
amejishindia Sh Milioni 1,000,000 baada ya kukopa kwenye taasisi hiyo ya
kifedha nchini.
Wateja
walioshinda katika bahati nasibu yetu na maeneo watokayo kwenye mabano
ni pamoja na Simion Ngassa (Iringa), Sisco Haule, (Kigoma), Said M
Mkinda (Dar es Salaam) na Phelis Nziku ambapo wote kila mmoja
watakabidhiwa kiasi hicho cha pesa kutoka Bayport Financial Services. Naye
Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo aliipongeza Bayport Financial Services
kwa kuendelea kubuni mambo yanayoweza kuwapatia mwanga wateja na
Watanzania kwa ujumla.
“Hii
ni bahati nasibu nzuri na rahisi kuchezwa na kila mtu, maana haina
vigezo zaidi ya mtu kuingia kwenye droo kama atakuwa amekopa tu, iwe
kwenye mtandao wao au kufika katika tawi la ofisi yao yaliyoenea sehemu
mbalimbali za Tanzania Bara,” alisema Ngolo, huku akiwataka Watanzania
kuendelea kunufaika na huduma mbalimbali za Bayport. Huduma
zinazotolewa na Bayport ni pamoja na mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa
mbalimbali kama vile vifaa vya ujenzi, bodaboda, injini ya boti,
pembejeo za kilimo, zikiwa ni miongoni mwa huduma zinazorahisisha maisha
kwa Watanzania wote.
picha na JIACHIE