Wachezaji watatu wa kimataifa
wanatua Azam FC kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chake, ikiwa ni sehemu
ya maandalizi ya ligi kuu Tanzania Bara na michuano ya Kombe la
Shirikisho barani Afrika.
Azam ilimaliza nafasi ya pili katka
msimu wa ligi uliokwisha na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania
katika michuano ya Shirikisho. Mmoja wachezaji hao ni mlinda lango
Mkameruni anayekipiga nchini Congo (DRC ), Nelson Lukong, anayetegemewa
kusaili usiku huu.Mbali na Nelson Lukong leo Alhamisi saa mbili asubuhi kiungo toka nchini England Ryan Burge atawasili na Qatar Air.
Jean Mugiraneze Babtiste toka nchini Rwanda anayekipiga na APR atawasili na Rwanda Air jioni ya leo Alhamisi
Baada ya mazoezi ya wiki tatu Azam FC inasafiri leo asubuhi kuelekea mjini Tanga, Kaskazini mwa Tanzania kucheza mechi mbili za kirafiki. Itacheza na African sports wana kimanumanu siku ya Jumamosi na Jumapili itakwaana na Coastal Union Mechi zote mbili zitachezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani majira ya jioni.
Timu itarejea Dar es Salaam siku ya Jumatatu.
na BBCSWAHILI
