
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya
Kikwete akiwasalimia wajumbe baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao
cha Halmashauri Kuu ya CCM, leo katika Ukumbi wa jengo la White House
mjini Dodoma. Kikao hicho ni cha kuchagua wagombea watatu kati ya watano
waliopitishwa na Kikao Cha Kamati Kuu ya CCM kwa ajili ya kuwania
kugombea Urais kwa tiketi ya CCM. Watatu watakaopatikana leo,
watapelekwa kuigiwa kura katika Mkutano Mkuu wa CCM ili kupata mgombea
mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo mkuu. Kushoto
ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni
Katibu Mkuu wa CCM,


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya
Kikwete (kushoto_ alipoingia ukumbini. Waliosimama mbele ni Wajumbe
waalikwa wa kikao hicho kutoka Baraza la Ushauri la Wazee Marais
wastaafu Ali Hassani Mwinyi na Benjamin William Mkapa na wengine ni
Makamu Wenyeviti wastaafu Mzee John Malecela na Mzee Pius Msekwa

Kikao hicho kikiendelea
YALIYOJIRI KABLA YA KIKAO HICHO

Aliyekuwa muomba kuteuliwa
kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, ambaye ameenguliwa, Edward Lowassa
akiwasili kwenye Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM kuhudhuria
kikao cha NEC.

Lowassa akiingia ukumbini

Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM
wa mikoa, Mzee Msidai akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini
kwenye kikao hicho cha NEC

Mjumbe wa NEC, Dk. Chegeni akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini

Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha, wa CCM, Zakiah Megji akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini

Aliyekuwa muomba kuteuliwa na CCM kuwania Urais, Steven Wasira akifuatwa na Waandishi wakati akiingiaukumbini

Kada wa CCM kutoka Zanzibar,
Mohamed Raza akizungumza na waandishi ambapo aliipongeza Kamati Kuu ya
CCM kwa kuweza kufanya uteuzi wa watu watano na kueleza kuwa inabidi
waliokosa kuteuliwa wawe watulivu kwa kuwa ndiyo Demokrasia

Muomba kuwania Urais kwa tiketi
ya CCM, Bernard Membe ambaye amefanikiwa kuingia tano bora, akizungumza
na waandishi kabla ya kuingia ukumbini kwenye kikao hicho leo

Muomba kuteuliwa kuwania Urais
kwa tiketi ya CCM, ambaye ameingia tano bora, John Magufuli,
akimsikiliza kwa makini mmoja wa wajumbe wa NEC, aliyekuwa
akimnong'oneza jambo kabla ya kuingia ukumbini

Waomba kuteuliwa kuwania Urais
kwa tiketi ya CCM ambao wamefanikiwa kuingia tano bora, Januari Makamba
na John Magufuli wakivheka kwa furaha walipokutana nje ya ukumbi kabla
ya kuingia kwenye kikao hicho.

Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Januari Makamba ambaye
amefanikiwa kuingia tano bora waliokuwa nje ya ukumbi wakati wa kikao
hicho

Wakuu wa vyombo vya habari vya CCM, Angel Akilimali (Uhuru FM) na Ramadhani Mkoma (Uhuru Publications Ltd

Muomba ridhaa ya CCM kuwania
Urais Bernard Membe akiwasalimia wajumbe ukumbini pengine kuomba kura
zao kabla ya kuanza kikao hicho

Waomba ridhaa ya CCM kuwania
Urais, ambao wamefanikiwa kuingia tano bora Bernard Membe na Dk. Asha
Rose Migiro wakisalimiana ukumbini wakati wa kikao hicho. Kushoto ni
Samwel Sitta ambaye pia aliomba nafasi hiyo lakini hakuingia tano bora

Aliyekuwa muomba kuteuliwa na CCM kuwania Urais, Lazaro Nyalandu ambaye hakuingia tano bora, akizungumza na Adam Malima

Wajumbe wakiwa ukumbini

"Usijai kaka" Katibu wa NEC,
Iikadi na Uenezi Nape Nnauye akimfariji aliyekuwa muomba rudhaa ya CCM
kuwania Urais, Mwiguku Nchemba, ambaye hakuingia tano bora.

"Usijai kaka" Katibu wa NEC,
Iikadi na Uenezi Nape Nnauye akimfariji aliyekuwa muomba rudhaa ya CCM
kuwania Urais, Mwiguku Nchemba, ambaye hakuingia tano bora.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Edward Lowassa ambaye hakpita tano bora, wakati wa kikao hicho.

"Naomba kura yako Ndugu yangu"
Bernard Membe ambaye amepitishwa na Kamati Kuu kuingia tano bora
akimsalimia Edward Lowassa ambaye amekosa kuingia tano bora, wakati wa
kikao hicho.

"Naomba kura yako Ndugu yangu"
Bernard Membe ambaye amepitishwa na Kamati Kuu kuingia tano bora
akimsalimia Edward Lowassa ambaye amekosa kuingia tano bora, wakati wa
kikao hicho

"Naomba kura yako Ndugu yangu,
tena napiga magoti" Bernard Membe ambaye amepitishwa na Kamati Kuu
kuingia tano bora akimsalimia Edward Lowassa ambaye amekosa kuingia tano
bora, wakati wa kikao hicho

January Makamba ambaye amefanikiwa kuingia tano bora akimsalimia Lowassa wakati wa kikao hicho cha NEC

Membe na Januari Makamba wakisalimiana ukumbini

Baadhi ya wajumbe ukumbini

Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mzee Sitta wakati wa kikao hicho cha NEC

Dk. Asha-Rose Migiro ambaye
amefanikiwa kuingia tano bora akimsalimia Lowassa na kumuomba kura
wakati wa kikao hicho cha NEC leo

Baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti wakiwa kwenye kikao hicho

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape
Nnauye kabla ya kuanza kikao hicho cha NEC