Jul 10, 2015

SERIKALI YA UJERUMANI YATIA SAINI HATI YA MAKUBALIANO NA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA KUSIMAMIA NA KUENDELEZA MALIASILI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhem Meru ( kulia) akiwa  na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Miradi la Ujerumani  la  Giz  nchini Tanzania,  Dkt. Sussane Grimm  ( kushoto)    wakitia saini  hati  ya Makubaliano  ya kusimamia na kuendeleza Maliasili nchini. Hafla hiyo fupi ilifanyika Jijini Dares Salaam, Makao Makuu  ya  Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House.


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhem Meru ( kulia) akiwa   na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la  Miradi la Ujerumani  la Giz  nchini Tanzania,  Dkt. Sussane Grimm  ( kushoto)    wakibadilishana  hati  ya Makubaliano  ya usimamizi na uendelezaji wa  Maliasili nchini. Hafla hiyo fupi ilifanyika Jijini Dares Salaam, Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House.


Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Miradi  la   Ujerumani  la Giz la  nchini Tanzania imetia saini  hati ya  makubaliano na  Serikali ya Tanzania kupitia  Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuendeleza na kusimamia Maliasili zilizopo nchini.

Hati hiyo ya Makubaliano   imesainiwa   na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhem Meru na  Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Giz  nchini Tanzania,  Dkt. Sussane Grimm .

 Utiaji saini huo umefanyika  Jijini Dares salaam,  Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House,  na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori , Bw. Herman Keryaro pamoja na baadhi ya  Maafisa  wa Wizara hiy.

Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Miradi  la   Ujerumani  la Giz  nchini Tanzania imeongeza kiasi cha Euro million tatu  sawa na billion kumi  kwa pesa za Kitanzania katika kusaidia usimamizi wa kiufundi ikiwemo  uanzishwaji wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini Tanzania ( TAWA) .   Pia Makubaliano hayo yatadumu kwa muda wa  miaka mitatu katika kusimamia na kuendeleza Maliasili nchini.

Uhusiano   kati ya Serikali ya Ujerumani  kupitia Shirika la Miradi  la   Ujerumani  la Giz  nchini Tanzania  na  Serikali  ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ulianza mwaka 2014.

Pia  Shirika la Miradi  la   Ujerumani  la Giz  nchini Tanzania imekuwa   ikishirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia  Wizara ya Maliasili na Utalii katika kipindi cha mpito cha Uanzishwaji wa Mamlaka ya Wanyamapori ( TAWA)  katika kuwandaa watumishi  kufanya kazi katika Mamlaka hiyo  
 
na JIACHIE