Mwigizaji mwenye jina kubwa ndani ya sanaa ya maigizo Bongo, Riyama Ally.
Mwigizaji mwenye jina kubwa ndani ya sanaa
ya maigizo Bongo, Riyama Ally amekiri kutamani maisha ya ndoa huku
akishikilia alichokisema ‘nasubiri wakati wa Mungu’.
Akizungumza na Amani
kwa njia ya simu hivi karibuni, msanii huyo mwenye sifa za kuvaa
uhusika wa huzuni na kulia katika filamu nyingi, alisema akiwa mwanamke
aliyekamilika, anahitaji kuwa na mume wake katika ndoa takatifu lakini
akaweka wazi kuwa kwa sasa ana mchumba ambaye anamuomba Mungu usiku na
mchana ili awe mumewe.
“Kila mtu aliyekamilika anahitaji maisha
ya ndoa, hakuna kitu chenye heshima katika maisha ya binadamu kama kuwa
na ndoa na kuishi kwa amani, lakini kila kitu hupangwa na Mungu.
Kiukweli kabisa natamani sana ndoa, nina mchumba ambaye namuomba Mungu
amfanye kuwa mume wangu,” alisema Riyama.