
MWENYEKITI
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho,
Abdulrahman Kinana, (kulia), akiwapungia wana CCM waliofika kumlaki
kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Julai 8, 2015.
Mwenyekiti
huyo wa CCM amewasili na kuanza kazi mara moja ya kuongoza kikao cha
kamati ya maadili ili kupokea taarifa za watia nia wa CCM, kabla ya
kuanza kuwajadili na kupunguza majina kutoka 39 hadi matano, kazi
itakayofanywa na Kamati Kuu ya chama hicho inayotarajiwa kukutana
Alhamisi Julai 9, 2015 majira ya usiku.
Baada
ya zoezi hilo la Kamati Kuu, majina hayo matano yatapelekwa kwenye
Halmashauti Kuu ya CCM, nayo itakaa na kuyapunguza tena na kufikia
majina matatu ambayo nayo yatapelekwa mbele hya wajumbe zaidi ya 2000 wa
Mkutano Mkuu wa chama hicho hapo Julai 12 na kuchaguz jina moja ambalo
ndilo litapitishwa nan kuwa mgombea wa CCM wa kiti cha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika
Oktoba 25, 2015


Rais
Kikwete, akisalimiana na viongozi wa juu wa chama hicho, makamu
mwenyekiti (Bara), Philip Mangula, Katibu Mkuu, Abdulrahmani Kinana,
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
chano JIACHIE