Watu watano miongoni mwao maafisa
wawili wa polisi wamefariki baada ya gari walilokuwa wakisafiria
kukanyaga bomu la kutegwa ardhini.
Watano hao walikua wakielekea mjini Lamu katika Pwani ya Kenya Kamishna wa jimbo la Garisa anasema kuwa maafisa hao walikuwa kazini wakielekea eneo la Hindi, kununua bidhaa za matumizi.
Mwandishi wa BBC aliyeko Garissa anasema kuwa gari hilo la serikali liliharibiwa vibaya katika shambulizi hilo la kwanza la aina hiyo.
Alisema kuwa bomu hilo lilikuwa limetegwa barabarani.
Hiyo ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa wapiganaji wa kigeni kupatikana miongoni mwa washambulizi wa kundi hilo baada ya mwili wa muingereza Thomas Evans ulipatikana.
