Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa ujambazi
waliovamia kituo cha Polisi cha Stakishari, Tazara,leo jijini Dar es
Salaam.
Naibu
wa Kamshina wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro akizungumza na
waandishi wa habari juu operesheni iliyofanyika ya kuwakamata
watuhumiwa wa ujambazi waliovyamia kituo cha Stakishari ,Tazara,jijini
Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova
akionyesha bunduki zilizoporwa katika uvamizi wa uliofanywa na majambazi
katika kituo stakishari,Tazara leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman
Kova akionyesha Fedha taslimu Sh.Milioni 170 zilizkutwa katika Shimo na
majambazi waliovyamia kituoa stakishaari na kuua askari,leo jijiji Dar
es Salaam.
Fedha
za watuhumiwa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakiki zikiwa
katika sanduku zikionyeshwa kwa waandishi habari na wananchi leo jijini
Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova
akionyesha picha za amajambazi sugu wanaotafutwa na jeshi la polisi
katika hafla ya kutuoa taarifa za kukamatwa kwa askari wa waliovamia
kituo cha stakishari leo jijini Dar es salaam
Pikipiki
zilizokuwa zikitumiwa na majambazi waliovyamia Kituo cha Stakishari
zikiwa mbele ya Kamisha Kova wakati akitoa taarifa kukamtwa kwao leo
jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAJAMBAZI waliovamia Kituo
cha Stakishari jijini Dar es Salaam watatu wauwawa na wawili watiwa
mbaroni wakati wakitupiana risasi katika eneo la Tuangoma ,Kigamboni
jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo la kukamatwa na kuuawa kwa majambazi hao lilitokea Julai 17 mwaka huu huko maeneo
ya Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, na majambazi wa tukio la kinyama la
kuuwawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari
wanakadiriwa kuwa kati ya 16 hadi 18.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam ,Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es
Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kukamatwa kwa majambazi hao inatokana na kikosi kazi kilichoundwa na kanda
maalumu kwa kushirikia na Mkoa Pwani.
Kukamatwa kwa watuhumiwa
hao wa ujambazi kulitokana na taarifa pamoja na mtego wa kiintelejensia katika
eneo la Tuangoma ndipo majambazi wakapita na pikipiki mbili walipowasimamisha
askari majambazi hao walikaidi amri nakisha kuanza kurusha risasi na polisi
wakajibu na majambazi watatu kuuwawa.
Majambazi waliouawa ni
Abbas Hashimu Mkazi wa Mbagala,Yassin alitambulika kwa jina moja mkazi wa
Kitunda Kivule, pamoja Saidi aliyetambulika kwa jina moja mkazi wa Mandimkongo
,Mkuranga.
Kamanda Kova amesema
wanaowashikiria ni Ramadhan Ulatule (15),Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga, Omary
Amour( 24) Mkazi Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.
Kova amesema baada ya
kuwabana watuhumiwa wa ujambazi walikwenda kuonyesha bunduki 15
walizopora katika kituo cha Stakishari ambazo walikuwa wamehifadhi chini ya
ardhi kuweka kinyesi juu.
Amesema katika Shimo
walilohifadhi walikuta bunduki aina Norinko ambayo wanatafuta ilipoibiwa pamoja
na kukuta fedha taslimu Sh.Milioni 170 za kitanzania.
Aidha amesema jeshi la
polisi limejizatiti katika matukio na kutaka watu waachane na biashara hiyo ya
ujambazi kuwa halipi.
Amesema fedha hizo
wanazichunguza kujua zimeibiwa wapi,na pikipiki mbili aina ya boxer nazo
wanazishiria na kutaka wauza pikipiki kuuzia watu ambao wanataarifa nazo.
“Hatutafumbia macho kwa
wale askari wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kuwachukulia hatua kali
ikiwa hata kama wanajihusiha na ujambazi tutawashughulikia kwani risasi
haichagui kuwa huyu raia au askari”amesema Kamishina Kova.
Tukio la kuawawa kwa askari
wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari,lilitokea julai 12
majira ya saa nne.
chanzo JIACHIE