Jul 19, 2015

MWENYEKITI WA ALBINO TANZANIA AJITOSA UBUNGE KOROGWE VIJIJINI, AAHIDI KULETA MAENDELEO

Mwenyekiti wa Chamacha Albino Tanzania (TAS), Bw. Ernest Kimaya (kushoto) akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walemavu wa Ngozi Tanzania kwenye viwanja vya Garden Mjini Iringa Mei 4, 2010. 
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania (Albino) ndugu Ernest Kimaya akimfariji Mama Maria Chambanenge wakati akipatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa kufuatia kukatwa mkono wake wa kushoto na watu walioshirikiana na mume wake na ambao walitiwa mbaroni na polisi mwaka 2013.
 Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania (Albino) Ernest Kimaya akisisitiza jambo kwa wanahabari kufuatia kuvamiwa na kukatwa mkono kwa Mama Maria Chambanenge wa mkoani Rukwa Februari 19, 2013.
 Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania, Ernest Kimaya, akitoa nasaha zake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Albinism Duniani katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Juni 13, 2015. 
Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma, wakiwa na Bw. Kimaya wakiwasikiliza watoto wenye albinism wakiimba wakati wa maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Albinism Dunia kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Juni 13, 2015.
Mwenyekiti wa TAS, Ernest Kimaya, akimpokea Rais Kikwete katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro Juni 12, 2015. Rais Kikwete ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Albinism Duniani jijini Arusha 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Bw. Ernest Kimaya akisoma nakala za Katiba Inayopendekezwa yenye maandishi yaliyokuzwa mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro Machi 15, 2015.
 
na JIACHIE