MWANDISHI wa habari
na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu
cha bibi k” ameamua kuingia kwenye
kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo la jipya la Ushetu katika halmashauri ya
wilaya ya Ushetu mkoani Shinyaga,kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na
maendeleo CHADEMA.
Bundala ametangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea
kuteuliwa na Chama ili aweze kupeperusha bendara katika uchaguzi mkuu ujao
katika mkutano wake wa kutangaza nia uliofanyika katika Kijiji cha Bogomba “B”
kata ya Ubagwe wilayani Kahama.
Mtia nia huyo alisema endapo Chama chake kitampitisha na
hatimaye kushinda Ubunge katika Jimbo hilo atahakikisha anasukuma kasi ya
maendeleo katika jimbo hilo jipya lenye Rasimali nyingi kupitia nafasi yake na
wajibu kama anavyotakiwa Mbunge Kufanya.
Alisema kuwa dhamira yake imemsuta kwenda
kuwatumikia wananchi wa wilaya hiyo ambayo yeye ni mzawa na kuwa atahakikisha anapigania
maendeleo ya wananchi kwa kasi huku akiondoa uonevu kwa waandishi wa habari na watumishi wengine serikalini na katika halmashauri za
wilaya.
maendeleo ya wananchi kwa kasi huku akiondoa uonevu kwa waandishi wa habari na watumishi wengine serikalini na katika halmashauri za
wilaya.
Sambamba na hayo amesema kuwa sababu nyingine iliyomsukuma ni
kuona wagombea wengine wanaolitaka jimbo hilo hawako kwa ajili ya ukombozi wa
jimbo hilo bali wako kwa ajili ya maslahi binafsi kutokana na asilimia kubwa ya wagombea hao si
wakazi wa eneo hilo na kwamba hawafahamu matatizo ya wana ushetu kama
anavyoyafahamu yeye.
Aliongeza kuwa akifaniiwa kuukwaa Ubunge pia atasimamia
kuhakikisha Jimbo hilo jipya linapata Chuo cha ufundi kwa ajili ya vijana wanaomaliza
darasa la saba na kidato cha nne kupata elimu jambo lilatalopunguza wimbi la
ukosefu wa ajira kwa vijana.
Bundala alisema kipaumbele kingine atakachoshughulikia ni
pamoja na kusimamia na kutoa elimu ya Sheria kupitia wanasheria ambao watazunguka
katika kata kutoa elimu hiyo hususan katika maswala ya umiliki wa
Ardhi,Mirathi,haki za wakulima na wafugaji pamoja na haki za raia na mali zao
kwa ujumla.
Akizungumzia kuhusu suala la michezo katika jimbo hili
Bundala amesema kuwa kupitia Kijukuu Cup atahakikisha anashirikiana na
halmashauri na wadau wa michezo kuhakikisha halmashauri ya ushetu inapata timu
ya kucheza ligi kuu Tanzania Bara.
Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CHADEMA (BAVICHA) Halmashauri
ya Ushetu Emmanuel Magema aliwataka vijana wote kuungana ili kumuunga mkono
kijana mwenzao aliyejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kuongoza akiwa Mbunge wa
jimbo hilo.
Wilaya ya Kahama kwa sasa ina halmashauri za wilaya tatu za
Msalala,halmashauri ya mji wa Kahama na halmashauri mpya ya Ushetu na kufanya majimbo ya uchaguzi kuwa matatu.
Katika kinyang’anyiro cha
Ubunge katika jimbo jipya la Ushetu kuna watu zaidi ya watano wanaotajwa
kulimendea jimbo huku wagombea wa CHADEMA wakionekana kuungwa mkono na makundi
mengi hususan vijana.
chanzo: kijukuu blog
