Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Core Securities Limited, Bw. George Fumbuka
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Umande
Unit Trust (UTT), mfuko wa uwekezaji wa pamoja utakaowawezesha wakezaji
wengi kukusanya mitaji yao kwa pamoja ili kupata mtaji mkubwa zaidi.
Ameambatana na Meneja uendeshaji wa kampuni hiyo Bw. Jonathan Swalala
(Kulia) na Meneja Mahusiano ya Wawekezaji, Bi. Sandra Felician
(kushoto). UUT ni mfuko wa pili wa pamoja kusajiliwa nchini, kufuatia
mfuko ulio chini ya serikali unaojulikana kama Dhamana ya uwekezaji
Tanzania (UTT).

Meneja
uendeshaji wa kampuni ya Core Securities Limited, Bw. Jonathan Swalala
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Umande
Unit Trust (UTT), mfuko wa uwekezaji wa pamoja utakaowawezesha wakezaji
wengi kukusanya mitaji yao kwa pamoja ili kupata mtaji mkubwa zaidi.
Ameambatana na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw. George Fumbuka
(wa pili kushoto) na Meneja Mahusiano ya Wawekezaji, Bi. Sandra Felician
(kushoto). UUT ni mfuko wa pili wa pamoja kusajiliwa nchini, kufuatia
mfuko ulio chini ya serikali unaojulikana kama Dhamana ya uwekezaji
Tanzania (UTT).
Kampuni
ya Core Capital Securities imezindua mfuko wa uwekezaji wa pamoja
uitwao Umande Unit Trust, utakaowawezesha wakezaji wengi kukusanya
mitaji yao kwa pamoja ili kupata mtaji mkubwa zaidi.
UUT
ni mfuko wa pili wa pamoja kusajiliwa nchini, kufuatia mfuko ulio chini
ya serikali unaojulikana kama Dhamana ya uwekezaji Tanzania (UTT).
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa UUT
Bw. George Fumbuka alisema kuwa wawekezaji wamepatiwa njia nyingine
iliyo salama na rahisi zaidi itakayowawezesha kuwekeza fedha zao.
“Faida
ya uwekezaji hutokana na ukubwa wake, yaani mtaji mkubwa huzaa faida
kubwa zaidi. Lakini pia hutokana na kusambazwa kwake katika mirija kadha
wa kadha ya uwekezaji,” alisema.