Idd Azan (mbele) akisalimiana na baadhi ya wanavikundi vya jogging.
.Idd Azan (kulia) akimsalimia muandaaji wa bonanza hilo, Aba Pelham.
Idd Azan (kulia) akimsalimia muandaaji wa bonanza hilo, Aba Pelham.
4..Picha ya pamoja ya wana-jogging wakiwa na Idd Azan.
Klabu za Joging zikiendelea kupiga picha na Idd Azan
Klabu nyingine ya jogging ikiwa katika picha ya pamoja na Idd Azan.
Iddi Azan akiwa amemshikilia kuku baada ya kuibuka mshindi.
Baadhi ya wanajoging wakimpongeza Iddi Azan mara baada ya kumkamata kuku huyo.
Wanajoging wakishindana kunywa soda.
Wanamama wakishindana kukimbia kwa kutumia magunia. 
Wanajogging wakishindana kuvuta kamba
Iddi Azan akiwa golini akidaka mpira kama ishara ya kufungua mashindano ya mchezo.
MBUNGE wa Kinondoni kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Idd Azan, anatarajiwa kuwa mlezi wa Klabu ya Jogging
ijulikanayo kwa jina la Kijitonyama Fitness Club.
Hayo yamesemwa na yeye mwenyewe alipokuwa
mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa klabu hiyo uliofanyika katika Viwanja vya
Masjid Qubah Kijitonyama, Dar, hivi karibuni.
Katika uzinduzi huo ulioandaliwa na Jamii
Sports Bonanza, kulihudhuriwa na vikundi vya jogging zaidi ya nane (8)
kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ambapo muandaaji wa
bonanza hilo alikuwa Aba Pelham.
Baadhi ya michezo iliyoshirikishwa siku
hiyo ilikuwa ni kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia kwenye magunia
huku pia mgeni rasmi huyo akishiriki vilivyo katika mchezo wa mpi
NA DENIS MTIMA/GPL