Muungano wa Ulaya EU umeanza kikao maalum kujadili uwezekano wa kukata
msaada wake nchini Burundi. Inakisiwa kuwa fedha kutoka muungano huo
unafikia zaidi ya nusu ya bajeti nzima ya Burundi ya kila mwaka.
Mkuu wa masuala ya kigeni wa Muungano wa EU Federica Mogherini,
ameelezea wasiwasi wake juu ya ghasia zilizototokea nchini humo kabla ya
kufanyika uchaguzi wa rais, na ametilia shaka iwapo serikali
itakayoundwa baada ya uchagzui huo itakuwa wakilishi ya taifa nzima.
Upande wa uchaguzi ulisusia kura hiyo iliyofanywa siku ya Jumanne. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Ijumaa hii.
Uamuzi
wa Rais Pierre Nkurunzinza kuwania urais kwa muhula wa tatu umetajwa
kwenda kinyume na mkataba waliosaini mjini Arusha miaka kumi na tano
iliyopita, ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mingi.
Ghasia zimezuka nchini humo tangu rais Pierre Nkurunzinza kutangaza
kuwania kiti hicho ambapo zaidi ya watu laki moja wamikimbia nchi hiyo
huku makumi ya maelfu wengine wakiuawa katika maandamano.
Juhudi kadhaa za kuleta upatanishi kati ya makundi hasimu zimeambulia patupu.
na BBCSWAHILI


