Na Mwandishi Wetu
Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa
waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwasilisha maombi yao
hadi mwishoni mwa mwezi huu (31 Julai, 2015).
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumatano, Julai 15, 2015) na
Mkurugenzi Mtendaji wa (HESLB) Bw. George Nyatega, hatua hiyo
imechukuliwa ili
kuwapa fursa wombaji ambao hawajakamilisha kufanya hivyo.
“Hatua
hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali
hawakuweza kufanya maombi ya mikopo katika muda uliopangwa,” amesema
Bw. Nyatega katika taarifa yake iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari.
Itakumbukwa kuwa awali Bodi ilianza kupokea maombi kwa njia ya mtandao (www.olas.heslb.go.tz) tarehe 4 Mei, 2015 na mwisho wa kuwasilisha maombi ulipangwa kuwa tarehe 30 Juni, 2015.
Kupitia
taarifa yake, HESLB imewataka waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo
2015/2016 ambao hawajakamilisha maombi yao kukamilisha na kuwasilisha
maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa na kusisitiza kuwa
hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 31 Julai, 2015.
HESLB
ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi
mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa
wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu.
