Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
imezindua huduma za mawasiliano ya simu za mkononi katika kijiji cha
Nduruma wilayani Arumeru mkoani Arusha na kuwawezesha wakazi zaidi ya
25,000 kupata huduma za mawasiliano.
Katika uzinduzi huo , Airtel pia ilitoa
msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule mbili za sekondari za Nduruma na
Sing'isi, vyenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 4 Akiongea wakati
wa uzinduzi wa huduma za mawasiliano, Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa
Airtel, Brighton Majwala alisema" Uzinduzi huu ni mwendelezo wa dhamira
yetu unaoenda sambamba na mipango ya serikali ya kutoa huduma za
mawasiliano kwa kila mtanzania.
Leo tunayofuraha kuwawezesha wakazi wa
vijiji vya Samaria, Majimoto na Maroran kupata huduma za mawasiliano za
uhakika, zenye ubora na za gharama nafuu huku tukiwawezesha kufanya
shughuli zao za kijamii na kiuchumi kwa ufanisi zaidi" "Tunaamini huduma
hizi za mawasiliano zitachangia katika kuboresha shughuli za kiuchumi
zikiwemo ufugaji, kilimo pamoja na biashara ambazo ni muhimu katika
kukuza uchumi.
Sasa wakazi wa Nduruma wamewezeshwa kupata
habari muhimu kupitia simu zao za mkononi wakati wotote na kwa urahisi
zaidi" Majwala aliongeza kwa kusema" Sambamba na uzinduzi wa huduma za
mawasiliano pia tumeweza kutoa vitabu vya sayansi kwa shule mbili za
sekondari wilaya hapa ili kuwawezesha wanafunzi na jamii kupata elimu
bora.
Tunaamini vitabu hivi pamoja na huduma hizi
za mawasiliano zitachangia kwa kiasi kikubwa k kubadili maisha ya wengi
na kuwawezesha watanzania na wakazi wa hapa kuzifikia ndoto zao". Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha , Fidelis Lumato ambaye
ndiye aliyezindua mnara huo na kutoa vitabu kwa shule za sekondari
alisema" tunayofuraha kupata huduma za mawasiliano kutoka Airtel hapa
Nduruma pamoja na vijiji vya jirani.
Hii ni nafasi ya pekee kwa wakazi wa hapa
kuboresha shughuli zao za kiuchumi na kutumia mawasiliano haya katika
kuboresha shughuli zao za kiuchumi na kijamii" "Serikali itaendelea
kuwaunga mkono Airtel katika jitihada zao za kuhakikisha inatanua wigo
wa huduma za mawasiliano na kufikia maeneo mengi hususani yaliyo
pembezoni mwa nchi.
Nawapongeza sana kwa juhudi hizi na kuwaasa
wakazi wa hapa kutumia fulsa hii katika kujiendeza na kuleta maendeleo"
Kwa upande wake, Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya sekondari Singisi ,
Hamad Boay alisema" Tunashukuru sana Airtel kwa kutupatia msaada huu wa
vitabu ambao utaboresha uwiano wa vitabu na idadi ya watoto shule ambapo
hapo awali kitabu kimoja kinatumika na wanafunzi watano, msaada huu
utaboresha uwiano ambapo kwa sasa mwanafunzi mmoja atatumia kitabu
kimoja.
Tunaahidi kuvitumia vizuri na kuvitunza
lakini zaidi wanafunzi wetu watafanya vizuri kimasomo na kutoa
wanasayansi bora shuleni hapa."
chanzo: Aitel Tanzania