Kundi la vijana katika mji wa Garissa ulioko Kaskazini Mashariki mwa
Kenya wameanza safari ya kutembea zaidi ya kilomita 700 kwa miguu
kuelekea mji wa Mandera katika mpaka baina ya Kenya na Somalia
ilikuchochea amani.
Vijana hao wa asili ya kisomali wanalenga kuhubiri amani na kuchochea
wenyeji wa eneo hilo lililoshuhudia mashambulizi mengi kutoka kwa kundi
la wapiganaji wa kiislamu la Al Shaabab.
Mwezi April wanafunzi
takriban 150 wa chuo kikuu cha Garissa waliuawa katika shambulizi baya
zaidi kuwahi kutekelezwa nchini kenya na kupelekea chuo hicho kufungwa.
Aidha waalimu na wafanyikazi wa umma kutoka maeneo mengine ya Kenya
wametoroka kutoka eneo hilo la Garissa , Wajir na Mandera wakihofia
usalama wao kufuatia mashambulizi yanayowalenga.
Shule nyingi za umma na hospitali zimeathirika pakubwa kutokana na kuhama kwao.
Vijana hao sasa wanalenga kuwahakikishia wenyeji na wageni kuwa eneo
hilo lina matumaini ya kurejea kwa amani ya kudumu na mtagusano baina ya
wenyeji na wageni.
Vijana hao wanalenga kukamilisha sfari hiyo katika kipindi cha siku 25 zijazo.
BBCSWAHILI

