
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi
wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani
Bw. Benjamin Thompson Kasenyenda akitoa wito kwa watanzania wote wenye
mapenzi mema kujitokeza kwa wingi kushiriki katika harambee hiyo
itakayofanyika katika viwanja vya Leaders club,siku ya Jumamosi Julai
4,2015 wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es
salaam.kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah
Mwambene.Kulia ni wajumbe wa Kamati hiyo Bi. Mwanamkasi Jumbe na Angela
Msangi.

Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwahamasisha
waandishi wa habari kuimarisha mshikamano katika Harambee ya kuwachangia
waandishi wa habari wanaosumbuliwa na magonjwa sugu ikiwemo
kansa.Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Grace Nakson.

Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa ambaye ni
mjumbe wa kamati ya kuratibu Harambee ya kuwachangia wanahabari
wanasumbuliwa na magonjwa sugu ikiwemo kansa akiwahamasisha wanahabari
wote nchini kuungana katika harambee hiyo kwa kuihamasisha jamaii
kushiriki katika tukio hilo muhimu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari
wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani Bw.
Benjamin Thompson.

Baadhi
ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa kuhamasisha kuwachangia
waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu
wa saratani.

Mjumbe
wa Kamati ya Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia
waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu
wa saratani Bi. Angela Msangi akiwahamasisha wanahabari kujitokeza kwa
wingi katika harambee hiyo na pia kutumia taaluma yao kuihamasisha jamii
kujitolea katika kufanikisha lengo la harambee hiyo. Kushoto ni Mjumbe
wa Kamati hiyo Bi. Mwanamkasi Jumbe.
PICHA NA FRANK MVUNGI-MAELEZO
chanzo. JIACHIE