Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano na Masoko,Consitantine
Magavila akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara
ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.kutoka kushoto ni msanii wa Bongo Fleva George Mdemu (Gnako),Afisa mipango wa kampuni ya Open Society Intiative for Eastern Africa(OSIEA),Adam Antony,Afisa Elimu NEC,Rose Malo pamoja na Snura Mushi(Snura).
Afisa
Elimu wa NEC,Rose Malo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na
vijana walioona umhimu wa kupiga kura na kuhamasisha vijana wengine kwa
njia ya nyimbo,kutokana na mwaka huu kuwa ni mwaka wa Uchaguzi mkuu hapa
nchini akizungumza katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo jijini Dar
es Salaam leo. kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano na Masoko,Consitantine Magavila na Afisa mipango wa kampuni ya Open Society Intiative for Eastern Africa(OSIEA),Adam Antony.
kutoka kushoto ni msanii wa Bongo Fleva George Mdemu (Gnako), Snura Mushi (Snura),Kala Masanja (Kala
Jeremiah) pamoja na Boniventure Kabogo(Stamina) wakiimba kipande cha
wimbo ambao utakuwa ukielimisha jamii kuhusiana na umhimu wa upigaji
kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria katika Mkutano wa wanaohamasisha
vijana kupiga kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu.(Picha na Avila
kakingo.)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
VIJANA
wamekuwa na changamoto ya kutoshiriki katika zoezi la kujiandikisha
katika daftari la kudumu la mpiga kura na kushindwa kupata haki yake
msingi ya kupiga kura katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini.
Kutokana
na kuwepo kwa hali hiyo Kampuni ya Mawasiliano na Masoko kwa
kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Shirika la Open Society
International pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wameanzisha
kampeni maalum kwa ajili ya kuhamasisha vijana kujiandikisha katika
daftari la wapiga kura katika mikoa ambayo daftari hilo halijapita.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Idara
ya habari Maelezo,Mmoja wa Wakurugenzi wa Mawasiliano na
Masoko,Consitantine Magavila amesema kuwa kampeni hiyo wasanii
mbalimbali wametengeneza nyimbo moja inayoenda kwa jina la Kuradili kwa
ajili ya kuhamasisha vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la
mpiga kura na hatimaye kupiga kura.
Amesema
wasanii walitunga nyimbo hiyo ni Gnako,Snura,Izo Biznez,Kala Jeremiah
pamoja na Stamina ambao watapita kutumbwiza katika mikoa ya Dar es
Salaam,Morogoro,Mwanza, pamoja na Shinyanga na hakuna kiingilio katika
matamasha hayo yaliyolenga kufikia watu milioni nne wakiwemo vijana.
“Vijana
wanaweza kuleta mabadiliko endapo watajitokeza katika kujiandikisha
katika daftari la kudumu la mpiga kura na hatimaye kupiga kura lakini
tumeona fursa yetu ni kuwahamasisha waweze kufanya hivyo”amesema
Magavila.
Nae
Afisa Elimu NEC,Rose Malo,amesema kujitokeza na kampuni hiyo itasaidia
vijana kuhaamasika kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kutokana
na ujumbe kutoka kwa vijana wenzao.