Kundi la Wabunge wa Hong Kong
wamenunua nafasi katika magazeti ya eneo hilo na kuwaomba wapiga kura
msamaha kwa kukosa kuwepo wakati kura muhimu ya kuamua hatma ya
kidemokrasia ya eneo hilo ilipopigwa bungeni siku ya alhamisi.
Wabunge
hao ni wale waliokuwa wanaunga mkono Serikali Kuu ya Uchina kuamua ni
nani anayepaswa kugombea kiti wakati wa uchaguzi mkuu ujao.Wabunge hao waliondoka bungeni kabla ya kura hiyo kupigwa katika juhudi za kuchelewesha uamuzi wa kupinga Uchina.
Hata hivyo hatua yao haikusaidia lolote kwa sababu wabunge wanaopinga Serikali kuu walishinda kwa wingi wa kura kuliko ilivyotarajiwa.
BBC
