Wanawake katika kijiji kimoja cha
kazkazini mwa Uganda wamefanya maandamano wakiwa uchi kutokana na
mgogoro wa ardhi kati ya utawala wa eneo hilo na jamii ambao umeendelea
kwa takriban miaka 10.
Wakati wa maandamano hayo ,mawaziri wa
serikali na watafiti walipanga kukata kipande cha ardhi katika kijiji
cha Apaa huko Amuru.Utawala wa wanyama pori nchini Uganda unaamini kwamba watu wanavamia ardhi ya uhifadhi wa wanyama pori huku wakaazi wakidai kwamba ardhi hiyo ilikuwa ya mababu zao.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa katika kabila la Acholi ,mwanamke anapovua nguo na kusalia uchi ni zaidi ya kupigana kwa kuwa inatoa laana kwa mpinzani wake.
chanzo BBC

