Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za ukomo wa utangazaji wa televisheni kwa mfumo wa analojia aliitaka TCRA kusimamia kwa ukamilifu maudhui kwenye vituo vyote vya runinga yanayowafikia wananchi ili yatumike kwa maendeleo .
Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhakikisha kuwa chaneli zote za runinga zinatoa mafundisho yanayoendana na maadili kwa ustawi wa maendeleo ya Taifa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa
sherehe za ukomo wa utangazaji wa televisheni kwa mfumo wa analojia
aliitaka TCRA kusimamia kwa ukamilifu maudhui kwenye vituo vyote vya
runinga yanayowafikia wananchi ili yatumike kwa maendeleo .
“Tuna changamoto ya kutengeneza maudhui ya ndani
(Local Content) ili tuweze kutangaza utamaduni wetu ndani na nje ya
nchi, kwa sasa mfumo wa dijitali umejaa maudhui mengi kutoka nje,”
alisema Dk Bilal.
Alizitaka taasisi husika kushirikiana na wadau
wote kutafuta mbinu bora na kutumia fursa ya mfumo huu kutengeneza
maudhui yatakayotangaza nchi, utamaduni, kukuza na kuimarisha amani,
utulivu na maendeleo.
Alizitaka taasisi za elimu nchini kutoa elimu kwa
njia ya runinga ili kurahisisha ufundishaji wa masomo mbalimbali
yakiwamo ya Sayansi na Historia.
Alisema anaamini taasisi hizo zikitoa elimu kwa
njia hiyo itakuwa rahisi kuwafikia wananchi wengi kwa wakati mmoja, pia
itapunguza gharama za ufundishaji.
Katibu Mtendaji wa Baraza la watumiaji wa
mawasiliano nchini, Mary Msuya amesema TCRA itafute teknolojia mpya ya
kuepuka uwapo wa utitiri wa ving’amuzi na badala yake itumike kadi moja
kwa ving’amuzi vyote.
Mkurugenzi wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema
Tanzania ina vituo vya runinga 28 na redio 104 lakini kutokana na
mabadiliko hayo ni dhahiri idadi itaongezeka.
Alisema changamoto kubwa ni kuhusu bei za
vin’gamuzi kwani ya chini ni Sh150,000 jambo ambalo wananchi wa hali
duni wanashindwa kuvimiliki na kuhusu matumizi ya king’amuzi kimoja,
suala hilo linahitaji maandalizi hivyo litachukua muda mrefu.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Profesa Makame Mbarawa alisema, wakati wanaanza mchakato wa kubadilisha
mfumo wa kuhamia dijitali, wananchi walidhani Serikali inawadanganya.
“Tulipozima mitambo hii kwa mara ya kwanza, Rais
Jakaya Kikwete alinipigia simu usiku saa moja kuniuliza inakuwaje
wananchi wanalalamika hivyo, nikamjibu natekeleza sheria, Rais akasema
Profesa endelea na kazi yako nikafurahi sana na leo nimefanikisha,”
alisema Makame.
chanzo: MWANANCHI
chanzo: MWANANCHI
