Jun 23, 2015

SERIKALI YA MAREKANI YAZINDUA MRADI WA DOLA MILIONI 14.5 WA KULINDA MAZINGIRA,KUKUZA UHIFADHI NA UTALII NCHINI TANZANIA

Balozi  wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa PROTECT  wa dola za kimarekani Milioni 14.5 wa kulinda mazingira,kukuza uhifadhi na utalii nchini hapa unaolenga kujenga uwezo wa uhifadhi na kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa wanyamapori nchini kote Tanzania,uzinduzi huu ulifanyika jana katika eneo la hifadhi ya wanyamapori linalosimamiwa na jumuiya ya uhifadhi ya wanyamapori {WMA} la Randilen linalopakana na hifadhi ya taifa tarangire Wilayani Monduli mkoani Arusha.
SAM_3306
Balozi  wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress wakitiliana saini mkataba wa mradi wa PROTECT na Waziri wa Mali Asili na Utalii nchini Tanzania Lazaro Nyalandu
SAM_3297
Waziri wa Mali Asili na Utalii nchini Tanzania Lazaro Nyalandu akizungumza katka uzinduzi huo, ameishukuru serikali ya Marekani kwa msaada huo huku akiongeza kuwa kumekuwa na uvamizi mkubwa katika maeneo ya hifadhi za taifa na kusema kuna mpango makakati wa kuhakikisha njia zote zinafunguliwa ili kuwezesha wanyamapori wote kuwa huru kuzunguka katika hifadhi zote nchini.
SAM_3282
Mkuu wa mradi huo wa PROTECT Jon Anderson akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa PROTECT  wa dola za kimarekani Milioni 14.5 wa kulinda mazingira,kukuza uhifadhi na utalii nchini hapa.