
Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba enzi za uhai wake.
Sehemu ya
wanawake waliofika nyumbani kwa Marehemu Mufti Alhaj Sheikh Shabaan Issa
Bin Simba Mikocheni B jijini Dar es Salaam leo.
Sheikh Mkoa wa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad
Mussa Salum akibadilishana na mawazo na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma Hassan Kiburwa
walipofika nyumbani kwa Marehemu Mufti ,Mikocheni B leo jijini Dar es Salaam .
Kulia
ni Sheikh wa Mkowa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akiwa
na baadhi ya Masheikh waliofika Nyumbani kwa Marehen Mufti,Shabaan Issa
Bin Simba Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.)
Na Chalila Kibuda.
MWILI wa
Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba unatarajiwa kusafirishwa kesho
mkoani Shinyanga.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania
(Bakwata),Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Alhaj Mussa Salum amesema mwili
wa marehemu utaswaliwa kesho katika Msikiti wa Msilimu ,viongozi mbalimbali wa
dini na serikali watakuwepo.
Amesema marehemU alikuwa akisumbuliwa na sukari,Shinikizo la Damu (BP) pamoja na Figo.
Hata hivyo amesema
kuwa jana (Jumapili) Mufti alifanyiwa oparesheni ya figo katika Hospitali ya TM
Jijini Dar es Salaam na Mauti ya Mufti yamekuta majira ya saa moja leo.
Salum amesema
marehem anatarajiwa kuzikwa Alhamis mkoani Shinyanga.
habari na jiachie blog