JAMII imeombwa kutoa msaada wa hali na mali kwa BI
GRACE KAIZA mkazi wa Igoma jijini Mwanza ambaye ameomba mukatwa mguu wake kutokana na Saratani ( Kansa) katika mguu huo.ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA KISA NA MKASA.
Akizungumza na *JEMBE Habari* Bi. Grace Kaiza amesema amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu jambo lililomuathiri kwa kiasi kikubwa kiafya na hata kiuchumi.
Akielezea namna tatizo hilo lilivyompata amesema lilianza kama uvimbe katika mguu wake kisha kufanyiwa upasuaji mara kadhaa lakini haikusaidia na ndipo alipobainika kuwa na ugonjwa huo.
Ameongeza kutokana na ugonjwa huo amekuwa akipata maumivu makali mno yanayo mliza hasa nyakati za usiku hali inayomfanya kushindwa kulala.
Naye msamalia mwema ambaye pia nimjumbe wa serikali ya mtaa wa NYAKATO MAHANGO Jijini Mwanza BI KHADIJA YASIN amesema kuna haja ya kumsaidia BI GRACE kutokana na shida anazopata
Fedha
inayohitajika ili kuweza kumsaidia BI GRACE Aaondokane na tatizo
alilonalo ni kiasi cha shilingi milioni mbili za kitanzania, ambazo
zitamwezesha kuondolewa mguu kabla haujaleta madhara zaidi.
Kwa
yeyote atakayeguswa na taarifa hii anaweza kuwasiliana na BI GRACE kwa
ajili ya kumsaidia kupitia namba za simu 0768 264 182
chanzo JEMBE FM MWANZA/Gsengo