pinzani nchini Afrika Kusini
unaitaka serikali imfute kazi mkuu wa polisi Riah Phiyega baada ya tume
maalum ya uchunguzi wa mauaji ya wachimba mgodi wa Marikana 2012
kuwalaumu kwa kusababisha vifo hivyo.
"ripoti hiyo iliwanyoshea
kidole cha lawama polisi na haswa Riah Phiyega kwa kuchukua hatua ambayo
walifahamu fika kuwa ingesababisha maafa"
Kiongozi wa chama cha upinzani Democratic Alliance Mmusi Maimane alisema katika taarifa hiyo.
Chama cha ''The Congress of the People'' (Cope) kilisema kuwa Phiyega
hafai kuendelea kuhudumu ''ilihali maafisa wa polisi walidanganya mara
mbili jopo hilo ''
Mauaji hayo yalitajwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo tangu ijinyakulie uhuru wake miaka 20 iliyopita.
Rais
Jacob Zuma ameliita tukio hilo kuwa baya zaidi kuwahi kutekelezwa na
polisi na kusema kuwa halina nafasi katika demokrasia ya taifa hilo.
Wafanyakazi
wa mgodi waligoma kwa siku kadhaa,na watu 10 tayari walipoteza maisha
wakiwemo watu ambao hawakuwa kwenye mgomo huo , walinzi wa mgodi na
polisi, kabla ya tukio hilo la tarehe 16 Agosti.
BBC

