Aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa
mataifa Koffi Annan amemtaka rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kujiuzulu
huku uchaguzi mkuu ukiahirishwa.
Kumekuwa na maandamano ya ghasia
nchini Burundi pamoja na mapinduzi yaliofeli tangu Nkurunziza atangaze
kuwa atawania muhula mwengine wa tatu wa urais katika kile watu wanaamni
ni ukiukaji wa katiba.Annan ameiambia BBC kwamba rais huyo amepoteza uhalali wake na sasa anafaa kujiuzulu iwapo anawajali raia wa Burundi.
Aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa
mataifa Koffi Annan amemtaka rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kujiuzulu
huku uchaguzi mkuu ukiahirishwa.
Kumekuwa na maandamano ya ghasia
nchini Burundi pamoja na mapinduzi yaliofeli tangu Nkurunziza atangaze
kuwa atawania muhula mwengine wa tatu wa urais katika kile watu wanaamni
ni ukiukaji wa katiba.Annan ameiambia BBC kwamba rais huyo amepoteza uhalali wake na sasa anafaa kujiuzulu iwapo anawajali raia wa Burundi.Uchaguzi wa Rais unatarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi Juni.
BBC