Jun 14, 2015

UBUNIFU WA KIVAZI CHA FAIZA ALLY CHAWAACHA WATU HOI

 Faiza Ally Msanii wa Filamu Tanzania akiwa amevalia kivazi cha aina yake "new style 2015''
ni katika ukumbi wa mlimani city wakati wa utoaji tuzo za Kilimanjaro musics awards 2015
 kivazi cha Faiza Ally kikiwa bado hakijavaliwa

Faiza akiwa tayari kwa mtoko wa Kilimajaro musics awards

Mwana mitindo na msanii wa filamu nchini Tanzania Faiza Ally amewashangaza wengi pale alipotinga nadi ya ukumbi wa mlimani city na kivazi cha pekee na cha aina yake 2015 haijawahi toke Faiza amesema ''hii ni stayle ya kipekee na muonekano wa tofauti kwa watu wengine na sio tu kila siku tuvae mavazi yale  ayele lazima tubuni mbinu mpya za mitindo angalau tusafishe njia za mitindo nchini kwtu na mataifa mengine yatambue kuwa wabunifu wapo wenye kuweza kufanya ubinifu yakinifu na wenye kuishangaza dunia kama wanavyofanya akina Kim Kardashian huko marekani''. Faiza ambaye ndio msanii pekee mwenye muonekano na mvuto wa tofauti na wasanii wengine kwa kila sherehe au function yoyote hapa nchini na nje ya nchi huwa anaonekana kuwa tofauti kabisa na wasanii wengi au raia wengine wanaokuwepo katika eneo la tukio kiukweli faiza ni mfano wa kuigwa na watu sasa wanatakiwa kumtafuta na awape mwongozo na ushauri wa mitindo kulingana na soko la ushindani wa mitindo linavyovuta kasi