
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye wameongoza makundi ya vijana kutoka Shirikisho la
Vyuo Vikuu pamoja na Machinga wa mjini Mwanza kukimbia mchakamchaka
(jogging) kwa umbali wa zaidi ya kilometa 2,kuanzia Barabara ya
Stesheni,kupitia barabara ya Posta,Kenyatta, Karuta,Lumumba maeneo ya
Soko Kuu mpaka Stendi ya zamani Tanganyika.
Viongozi
mbali mbali walishiriki mchakamchaka huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mhe. Magessa Mulongo,Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Masoor na
Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana akikimbia mchaka mchaka
(jogging)katika mitaa ya jiji la Mwanza ,wengine pichani ni Katibu wa
CCM wilaya ya Nyamagana Mpanda(kushoto),Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza
Ndugu Miraji Mtaturu na wa mwisho kulia ni Mwenezi wa CCM mkoa wa Mwanza
Magelepa.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana walioshiriki
mchakamchaka (jogging) na kuwataka kuendelea kufanya mazoezi kwani
yanasaidia kuimarisha afya na kujenga mwili.