KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE LEO
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiteremka kwenye basi
kuwasalimia wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wa mkoa wa
Morogoro akiwa njiani kuelekea mkoani Kagera.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa mkoa wa
Morogoro waliojitokeza kuwasalimu wakati wa safari ya kuelekea Kagera.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi waliojitokeza
kwenye kituo cha mabasi mjini Morogoro maarufu kama Msamvu ambapo
aliwaambia wananchi hao huu ni wakati wa kuchagua kiongozi wa kutuongoza
hivyo ni vyema wananchi kupima na kuacha ushabiki.