Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez
(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati
wa hafla fupi ya kutiliana saini mkataba wa kusisaidia Hospitali hiyo.
Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans na Daktari Bingwa wa Mifupa wa Hospitali hiyo, Prosper Alute.
Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans akizungumza katika hafla hiyo.
Meneja
Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (wa pili kushoto), akibadilishana hati
na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Hospitali ya CCBRT baada ya kutiliana
saini mkataba wa kusaidi matibabu ya ulemavu wa miguu Dar es Salaam
jana. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Mifupa wa Hospitali hiyo, Prosper
Alute na Meneja Uwajibikaji kwa Jamii, Woinde Shisael.
Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanja (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Picha mbalimbali zikionesha miguu iliyopinda.
Wanahabari wakiwa kwenye hafla hiyo.
Joyce
Moshi akiwa amembeba mtoto wake Gedion ambaye anatibiwa katika
Hospitali hiyo kutokana na miguu yake kupinda ambapo sasa anaendelea
vizuri.
Na Dotto Mwaibale
HOSPITALI
ya CCBRT, imepokea dola 150,000 (zaidi ya sh. mil. 320) kutoka kwa
Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kwa ajili ya kugharamia matibabu ya
watototo wanaozaliwa na ulemavu wa nyayo zilizopinda kwa miaka mitatu
ijayo.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema hiyo
si mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kugharamia matibabu ya walewavu kwani
miaka mitatu iliyopita pia waligharamia matibabu ya watoto wenye
ulemavu wa midomo.
"Tuna
amini watoto wenye ulemavu wa unyayo uliopinda watapatiwa matibabu
mapema, hivyo tunaomba wazazi wenye watoto wao wanaozaliwa na ulemavu
huo kujitokeza CCBRT kupatiwa matibabu kwani ni bure na kwa mwaka
tunatoa dola 500," alisema Gutierrez.
Kwa
upande wa Daktari wa Mifupa wa hospitali hiyo, Prosper Alute
akizungumzia ugonjwa huo, alisema unasababishwa na kurithi kutoka kwa
wazazi au ndugu na kunywa pombe kupindukia au kutumia dawa zenye
viambata kali.
Alisema
asilimia 50 ya watoto wanaozaliwa hupata ugonjwa huo kwa miguu yote
ambapo tangu kuingia kwa mwaka huu hadi Aprili, watoto 117 wamegundulika
kuwa na ugonjwa huo ambao ni sawa na wastani wa watoto 10 kwa wiki.
Alisema ugonjwa huo usipotibiwa kwa haraka unaweza kumsababishia mtoto kutembea kwa shida na wakati mwingine kutotembea kabisa.
Kwa
upande wa Joyce Mosha, Mkazi wa Mwenge, ni mmoja wa wazazi ambaye
mtoto wake, Gidion ana miezi miwili alikutwa na tatizo hilo na kufanyiwa
upasuaji, alisema mara baada ya kujifungua madaktari waligundua mtoto
wake kuwa na tatizo hilo, hivyo waliamua aanze kupatiwa matibabu.
"Namshukuru
Mungu alifanyiwa upasuaji mdogo na hivi sasa anaendelea vizuri,
alipogunduliwa ana tatizo hilo kwanza walimfunga plasta ngumu (POP) kwa
wiki tano na kisha kumfanyia upasuaji mdogo wa mfupa na kumpa viatu
maalumu vya kuvaa na vingine huwa anavaa usiku tu wakati wa kulala,"
alitoa ushuhuda Joyce.
chanzo: JIACHIE BLOG