Mkutano
wa Mabalozi wa Tanzania ulioanza Mei 25-27, 2015 katika hoteli ya
Ramada, Dar es Salaam. Lengo kuu la mkutano huo ni kujadili utekelezaji
wa Sera ya Mambo ya Nje na mchango wa Wizara kufikia Dira ya Taifa 2025.
Mkutano huu ni wa nne kufanyika tangu ule wa kwanza uolifanyika mwaka
1999 katika hoteli ya Whitesands, Dar es Salaam.
Kauli
mbiu ya mkutano ni Diplomasia ya Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025.
Ujumbe huo umechaguliwa kwa kuzingatia mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa katika juhudi za kutimiza ndoto ya kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (wa pili kutoka kushoto) akiongea wakati wa Mkutano wa Mabalozi wa
Tanzania ulioanza Mei 25-27, 2015 katika hoteli ya Ramada, Dar es
Salaam. Kutoka kulia ni Balozi Liberata Rutageruka Mulamula ambaye
ameziwakilisha nchi za Marekani na Mexico ambaye pia ni Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim
pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India, Engineer John Kijazi ambaye
anawakilisha nchi za India, Sri Lanka, Singapore na Nepal.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa Balozi
Yahya Simba akitoa shukrani kwa viongozi waliweza kufanikisha mkutano
huo.