
WATU
KUMI NA TANO WAJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA BASI LA ABIRIA MALI YA
KAMPUNI YA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.791 BZR AINA YA NISSAN
LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE SALUMU SELEMANI (45) MKAZI WA
D’SALAAM KULIGONGA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.778 CAN ISUZU FTR
LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE EDWIN LUYENGA (40) NA KISHA KUGONGA KWA
NYUMA GARI T.565 CVB/T.836 BBC AINA YA MAN LILILOKUWA LIMEHARIBIKA NA
KUEGESHWA.
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 10.05.2015 MAJIRA YA SAA 20:10 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA KAPYO, KATA YA MAHONGOLE, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA
MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE.
MAJERUHI
KATIKA AJALI HIYO NI WANAUME TISA [09] NA WANAWAKE SITA [06]
WALIFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. APAMAT UMUYU (41) MKONGO 2. SALUMU RASHIDI
(29) MKAZI WA DSM 3. JUMA RAJABU (34) MKAZI WA ZANZIBAR 4. ANNA
MISIKITA (36) MKONGO 5. DAVID MTACHI (43) MKAZI WA DSM 6. GROLI AMANI
(41) MKAZI WA DSM 7. KELVIN JORDAN (39) MKAZI WA DSM 8. WAZIRI OMARY
(35) MKAZI WA DSM 9. MCHEMBE GEORGE (35) MKAZI WA MWANZA.
MAJERUHI
WENGINE NI 10. LIKA ILUNGA (47) MKAZI WA KONGO 11. MAJARIWA RAMADHANI
(51) MKAZI WA KAGERA 12. ADELA MUTOMBA (46) MKAZI WA KONGO 13. MUDY
ABDALLAH (43) MKAZI BUKOBA 14. NASORO MKAZI WA TANGA, MAJERUHI MMOJA
MWANAMKE AMETIBIWA NA KURUHUSIWA NA WENGINE 14 WAMELAZWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA BASI AMBAYE AMEKAMATWA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R.
WANKYO ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA SHERIA/KANUNI/ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.