Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto
Nyusi akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini
Dodoma huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika wa Bunge hilo
Mh.Anna Makinda wakisikiliza.
Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto
Nyusi akipokea heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya
Bunge mjini Dodoma akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete.
Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto
Nyusi akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania leo huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika
Mhe.Anna Makinda wakishuhudia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
mgeni wake Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi, Waziri Mkuu Mizengo
Pinda,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi
waandamizi katika serikali ya Msumbiji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Rais wa Msumbiji kulihutubia Bunge mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete akimtambulisha katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana kwa Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi wakati Rais huyo wa
Msumbiji alipowasili katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma na
kuzungumza na viongozi waandamizi. Kushoto ni Naibu katibu Mkuu wa CCM
Bwana Mwigulu Nchemba.
(Picha na Freddy Maro)