Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani
Athumani Msuya, kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai
(Director of Criminal Investigation).
Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu
Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai. CP Msuya anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye amestaafu kwa
mujibu wa Sheria.
Rais Kikwete pia amemteua Naibu Kamishna wa
Polisi (DCP) Valentino Mlowola kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai,
kujaza nafasi inayoachwa na Kamishna Msuya.
Kabla ya Uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza. Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015.
Imetolewa na;Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Mei, 2015