Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa (watatu
kushoto mstari wa nyuma) akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya mradi
wa mawasiliano vijijini Awamu ya 2B ambapo makampuni ya simu ya TTCL,
Vodacom na Tigo walisaini. Wanaosaini kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji
Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano Injinia Peter Ulanga, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na
Uhusiano wa Vodacom,Rosalynn Mworia na Mwakilishi wa kampuni ya MIC,
Slyvia Balwire. Sherehe hiyo ilifanyika mkoani Dodoma jana.
Afisa
Mkuu Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Injia Peter Ulanga
akibadilishana hati za makubaliano na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na
Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia mara baada ya kusaini
mkataba wa kupeleka mawasiliano ya simu vijijini, katika sherehe
zilizofanyika mjini Dodoma leo.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (katikati)
akiwa na Wawakilishi wa makampuni ya simu yaliyosaini mkataba wa
kupeleka mawasiliano ya simu vijijini sherehe iliyofanyika mjini Dodoma
jana. Wengine ni Mwakilishi wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano, Aumsuri
Moshi (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano Injinia
Peter Ulanga. Mstari wa nyuma ni wawakilishi wa makampuni hayo ya simu,
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura, Mwakilishi wa Vodacom
Tanzania, Rosaline Mworia na Mwakilishi wa MIC Tanzania Ltd, Sylivia
Balwire.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Prof Makame Mbarawa,(pili
kushoto) akiwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom
Tanzania Rosalynn Mworia mara baada ya kampuni ya Vodacom kuwa kati ya
makampuni matatu yaliyo saini mkataba wa kupeleka huduma ya mawasiliano
simu vijijini awamu ya 2B katika sherehe zilizofanyika mjini Dodoma leo.
chanzo: michuzi media