Polisi ya Burundi imetangaza kuwa, mbali na polisi hao wawili, mtu mmoja mwengine alipoteza maisha katika shambulio hilo lililotokea jana usiku jijini Bujumbura. Kwa mujibu wa mashuhuda, shambulio hilo lilitokea majira ya saa moja na nusu usiku katika eneo la Kamenge, kaskazini mashariki mwa mji huo.
Maandamano ya kupinga uamuzi wa Rais Nkurunziza kutaka kugombea katika uchaguzi wa rais ujao, yamezorotesha uchumi wa nchi hiyo. Hayo yanajiri katika hali ambayo rais huyo ameendelea kushikilia msimamo wake wa kugombea kwenye uchaguzi huo.
Akihutubia sherehe za Mei Mosi hapo jana, Rais huyo kijana, mbali na kukosoa maandamano ya wapinzani aliwataja watu wanaoandamana kuwa ni watoto wadogo wanaojiingiza katika mambo yasiyowahusu.
chanzo GPL