Mkurugenzi
wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza
kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha Shirika hilo
uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo hicho kilichopo Makao makuu ya
Shirika barabara ya Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam,
Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii,
Susan Omari.

Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wanaoshuhudia tukio hilo .

Maofisa
wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa
Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho
inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.

Mkurugenzi
waShirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza

Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa
Jamii, Susan Omari.

Maofisa
wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa
Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho
inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.

Maofisa
wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa
Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho
inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.

Wakurugenzi wa Shirika hilo wakishuhudia tukio la kuzinduliwa kwa tukio hilo

Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wanaoshuhudia tukio hilo .
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA KWA NJIA YA
SIMU NA MALIPO YA KODI KWA MFUMO WA SIMU ZA KIGANJANI – MEI 19, 2015
.................................................................................................
Katika jitihada za Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC) kuboresha huduma kwa wateja kama ilivyoainishwa kwenye
Mkataba wa Huduma kwa Mteja, leo Shirika la Nyumba la Taifa linazindua
huduma mbili, ambazo ni kituo cha huduma kwa wateja na pili ni mfumo wa
kulipa kodi za nyumba kwa kutumia simu ya kiganjani.
Kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya
simu kitatumika kuhudumia wateja wetu wote kwa kupiga simu pale
wanapohitaji kufahamu juu ya huduma zetu na bidhaa mbalimbali pamoja na
kutoa taarifa mbalimbali za shirika zinazohusu huduma kwenye makazi yao.
Wateja wataweza kupata huduma hii kupitia nambari
+255 784 105 200
na + 255 222 162 800. Kupitia kituo hiki Shirika linawaahidi kwamba
maulizo na taarifa zozote zitakazoripotiwa zitapewa kipaumbele kwa
kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
Katika kuendelea kuboresha mfumo wa
ukusanyaji kodi kutoka kwa wapangaji wetu, Shirika limeanzisha mfumo wa
kulipa kodi kupitia simu za kiganjani ili wapangaji waweze kufanya
malipo ya kodi zao bila ya usumbufu wowote kupitia tigopesa, mpesa na
airtel money. Kupitia mfumo huu, wapangaji wataweza kufanya malipo kwa
kutumia simu zao na wataweza kuhamisha fedha kutoka kwenye benki akaunti
zao na kwenda Shirika la Nyumba mahali popote walipo na kwa muda wowote
ambao ni muafaka kwao bila ya kufika katika vituo vyetu vya makusanyo
ya kodi.
habari na GPL