May 14, 2015

NEEMA NGASHA MSANII WA INJILI MWENYE SAUTI YA PEKEE KABISA TANZANIA

 Neema Ng'asha muimbaji wa Injili





 Msanii maarufu njini Neema Ng'sha amekuwa nguzo kubwa na muhimili katika kulisukumba gurudumu la sanaa ya injili hapa nchini tanzania. muimbaji huyu nguli mwenye maskani yake jiji dar es salaam amekuwa nambari moja katika kushirikishwa na kusindikiza uzinduzi mbali mbali wa matamasha ya injili hapa Tanzania na nje ya tanzania na raia wengi wa madhehebu ya kikristo yamekuwa mstari wa mbele kuweza kumfatilia kwa ufasaha zaidi katika kazi zake za uendeshaji wa huduma ya injili makanisani na hata nje ya makanisa Neema tayari amekwishatoa baadhi y nyimbo zake zinazosikika katika vituo mbali mbali vya rediopamoja na kusambaza kazi zake CD/DVD madukani na watu wengi wamekwishapata copy za kazi zake.

 wasanii wengi wa injili wameonekaa kuwa bize na kazi zao na hata imefika hatua wameisahau jamii inayowazunguka na hata kuweza kutoa misaada katika vituo vya watoto yatima na kwa watu wasio jiweza lakini mwanadada huyu mtumishi wa mungu ameisaidia sana jamii kwa kujitolea katika kufanikisha malengo ya jamii kwa ushauri kwa vijana misaada mbali mbali mbali katika vituo vya kulelea watoto yatima na hivyo imepelekea jamii kubwa kumkubali na kumtaka sasa afanye kazi aliyotumwa na mungu na mwisho wake atayaona matunda yake ''hakika alilolipanga mwenyezi mungu hakuna wa kulikatisha'' {Neema Ng'asha }