Raisi
wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba(katikati) akielezea
jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati alipokutana nao katika
ofisi zake kuelezea siku ya tuzo za filamu zitakazofanyika jumamosi hii
jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Bwana Ezekiel kutoka Push Mobile na
kushoto kwake ni Meneja Masoko wa EATV na EAR Happy Shame.
Meneja
Masoko kutoka EATV na EA Radio Happy Shame(kulia)akielezea jambo kwa
Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba wakati wa
mkutano na wana habari kuhusu Tuzo za Filamu Tanzania 2015 leo jijini
Dar es Salaam ambapo EATV na EAR ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo.
Mei 23, hapatoshi Mwalimu Nyerere Internnational Conference Center;
Ni
siku moja tu imebaki kufanyika kwa tuzo kubwa za filamu nchini
‘Tanzania Film Awards’ 2015(TAFA). Ni tuzo kubwa ambazo zitafanyika kwa
mara ya kwanza jijini Dar es Salaam tarehe 23 Mei 2015, Mwalimu Nyerere
International Conference Center. Haya
ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu nchini na kila mmoja ana
shauku ya kushuhudia tuzo hizo zitakazo wapa wasanii wetu amsha amsha ya
mafanikio katika tasnia yao.
Akiongea
na wana habari katika ofisi zake raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania
Simon Mwakifwamba alisema, “Maandalizi yote yapo tayari na tumejipanga
kikamilifu kufanikisha tuzo hizi. Kutakuwa na burudani mbalimbali
kusherehesha tuzo hizi zikiongozwa na mzee Kikii, Mwasiti na Barnaba,
pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wana tasnia ya filamu
watakaowakilisha vizuri kabisa tasnia yao kwa kutufanya tucheke na
tufurahi.
Yote
hii ni kuwaburudisha wageni wetu watakaokuja kutuunga mkono katika siku
hii muhimu kwa wana tasnia ya filamu.Tuna wageni mbalimbali ambao
wameshafika kutoka nchi tofauti za Afrika ili kutuunga mkono katika
hafla hii”.
“Napenda
kuwashukuru waisani mbalimbali waliojitolea kutuunga mkono Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, TRA, EATV na EAR, International
Eye Hospital, Foreplan Clinic, R&R Associates, Simu Tv na Barazani
Production. Kwa namna ya pekee nashukuru vyombo vyote vya habari kwa
sapoti kubwa waliotupa kipindi chote cha mchakato wa tuzo hizi tangu
wakati wa uzinduzi hadi sasa bado wapo nasi bega kwa bega.”
“Wito
wangu kwa watanzania na wana Afrika Mashariki kwa ujumla kutuunga mkono
kwa kununua tiketi za hafla hii ili waweze kufika kushuhudia tuzo hizi
za kipekee zitakazo andika historia mpya katika tasnia ya filamu.
Tiketi
zinapatikana kwa bei ya 50,000/= kawaida na VIP ni 100,000/= katika
vituo vifuatavyo;Shear Illussion - Mlimani City and Millenium Towers,
Robby One Fashion- Kinondoni and Sinza Africasana, B&B Boutique- Dar
Free Market duka namba 46 na Viva Towers duka namba 31, Secky Bureau de
Change - Big Bon Sinza Mori, Save Mart wholesalers - Mikocheni kwa Nyerere EATV na ITV. Karibuni sana tufurahie na kuunga mkono kazi za wasanii wetu.” Alisisitiza Mwakifwamba.
Tuzo
za Filamu Tanzania 2015 zitakua na ‘surprises’ za kutosha hasa
kushuhudia mastaa kutoka nchi za Ghana na Nigeria na mengine kibao. Watanzania wajitokeze kwa wingi kuunga mkono kazi za wasanii wetu hii ni kuonesha uzalendo kwa kupenda kazi za wasanii wetu.