Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (kulia) akizungumza na
Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini
Magharibi pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya
usambazaji umeme vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo (hawapo
pichani). Katikati ni Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Nyanda za
Juu Kusini Magharibi, Salome Nkondola na kushoto ni Kaimu Meneja wa
Tanesco katika mkoa wa Mbeya, Magwila Mbalamwezi.
Meneja
Tanesco katika wilaya ya Mbozi mkoa wa Mbeya, Ephraim Cheyo
(aliyesimama) akieleza kuhusu utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme
vijijini katika wilaya yake, wa kwanza kushoto ni Meneja Tanesco, wilaya
ya Kyela, George Fulla na wa pili kushoto Meneja Tanesco katika wilaya
ya Mbinga, Kanuti Punguti. Maelezo hayo aliyatoa wakati wa kikao
kilicholenga kujadili utekelezaji wa miradi ya usambazaji vijijini
katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi kilichofanyika jijini
Mbeya.
Mameneja
Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja
na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme
vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo wakimsikiliza kwa makini Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (aliyesimama) katika kikao
kilichofanyika jijini Mbeya ili kujadili utekelezaji wa miradi ya
usambazaji umeme vijijini katika kanda hiyo.
Mameneja
Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi,
wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini
Awamu ya Pili katika kanda hiyo pamoja na watumishi wa Wizara ya Nishati
na Madini, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles
Mwijage (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika jijini Mbeya ili
kujadili utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini katika kanda
hiyo.
picha michuzi blog