Waandamanaji nchini Burundi wakifanya vurugu kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais wa awamu ya tatu.
Raia mmoja amefariki dunia na wengine
tisa kujeruhiwa katika maandamano yanayoendelea kupamba moto nchini
Burundi kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula
wa tatu.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anayetarajia kuwania urais wa awamu ya tatu nchini humo.
Taarifa zinasema kuwa, mamia ya watu wamejitokea kwenye maandamano hayo huku wakichoma moto baadhi ya vitu.
Siku ya jumanne wiki hii, Mahakama ya Katiba nchini Burundi ilikubali
kuwa Rais Nkurunziza anaweza kugombea urais ambapo ilisema ni halali
yeye kuwania tena urais kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Katika hotuba yake siku ya jumatano Rais Nkurunziza alisema kama
atachaguliwa tena kuongoza nchi hiyo, muhula huu utakuwa wa mwisho kwake
kuwa madarakani.