Wanausalama wameeleza kuwa Yusuf Dirir aliuawa baada ya gari lake kushambuliwa na wanamgambo wanaodhaniwa kuwa wa Kundi la Al Shabaab.
Takribani wabunge watano waliuawa na Kundi la Al Shabaab mwaka jana huku kundi hilo likidai kuendeleza mauaji dhidi ya wabunge.
Kundi hilo jana Jumamosi lilipambana na vikosi vya majeshi ya serikali katika Wilaya ya Awdigle na Kijiji cha Mubarak kusini mwa Mji wa Mogadishu.
Katika mapigano hayo, takribani watu 17 wameripotiwa kupoteza maisha.
chanzo:GPL