Shughuli ya upigaji kura inaendelea
huko Ireland katika kura ya maoni ya kubadilisha katiba ili kuruhusu
ndoa za mapenzi ya jinsia moja.
Iwapo mabadiliko hayo
yataidhinishwa,Ireland itakuwa nchi ya kwanza kuhalalisha ndoa za
wapenzi wa jinsia moja kwa wingi wa kura.Matokeo ya kura hiyo yanatarajiwa jumamosi mchana.
