Meneja Masoko wa Kampuni ya
Huawei Tanzania, Lydia Wangari akizungumza na waandishi wa habari jana
katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha TEKU mara baada ya kuzindua bonanza la
wafanyakazi wa mabenki lililoandaliwa na Real Brand Solutions Ltd na
kudhaminiwa na Huawei.
Baadhi ya wafanyakazi wa mabenki mkoani Mbeya wakipata huduma katika vibanda vya Huawei.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Huawei
Mkoa wa Mbeya na Nyanda za Juu Kusini, Polyne Msuya (kulia) akitoa
maelezo kwa wadau waliotembelea banda hilo katika Viwanja vya Chuo Kikuu
cha TEKU jijini Mbeya ambapo Huawei ndiyo walikuwa wadhamini wakuu wa
bonanza hilo.
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa
Kampuni ya Real Brand Solutions Ltd ambao ndiyo waandaaji wa bonanza
hilo, Innocent Mafuru akiongea na wanahabari wakati wa bonanza hilo
lililofanyika jana.
Timu za soka za wafanyakazi wa Benki ya Posta na Benki Kuu (BOT) wakimenyana katika bonanza hilo.
Mwenyekiti wa UVCCM Mbeya, Amani
Kajuna (mwenye shati la mistari) akifurahia jambo na Polyne Msuya mara
baada ya kutembelea banda la Kampuni ya Huawei kujionea simu za kisasa.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB na CRDB wakimenyana katika mpambano wa mpira wa kikapu
chanzo: GPL