May 31, 2015

DK. SLAA AVISHWA VAZI LA KICHIFU, APEWA JINA LA 'MWENE WA MBOZI' HUKO MBOZI MKOANI MBEYA

Kiongozi wa Machifu wa Kabila la Wanyiha, Greenwell Msangawale akimvisha vazi maalum la kichifu Dk.Slaa.
Kiongozi wa Machifu wa Kabila la Wanyiha, Greenwell Msangawale akiongea na wananchi wa Mbozi baada ya zoezi hilo.

Dk. Slaa akivishwa vazi hilo.
Dk. Slaa akiwa na mundu aliyokabidhiwa na Kiongozi wa Machifu wa Kabila la Wanyiha, Greenwell Msangawale.
KIONGOZI wa Machifu wa Kabila la Wanyiha, Greenwell Msangawale amemvisha vazi maalum la kichifu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa na kupewa jina 'Mwene wa Mbozi' ambapo pia alikabidhiwa silaha ya jadi aina ya mundu wakimtuma kazi ya kuendeleza vita dhidi ya ufisadi na ubadhirifu nchini ambao umekuwa moja ya sababu za umaskini wa Watanzania.
Tukio hilo limefanyika kwenye Uwanja wa Ichenjezya, Vwawa, wilayani Mbozi, Mkoa wa Mbeya ambapo kiongozi huyo amefanya mkutano wa hadhara baada ya kukagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa BVR.
(PICHA ZOTE NA CHADEMA)