
Pichani
ni sehemu ya barabara kutoka Bamaga kuelekea Afrikasana Sinza jijini
Dar ikiwa hoi bin taaaban baada ya kufunikwa na maji kufuatia mvua
ambazo zimekuwa zikiendelea kunyesha jijini,aidha mafuriko hayo yamekuwa
yakisababishwa pia na mitalo mingi ya eneo hilo kuzibwa na takataka
zinazotupwa holela,matokeo yake maji yamekuwa yakikosa muelekeo.Idara
husika wanapaswa kulifanyia kazi ipasavyo eneo hilo kwani limekuwa ni
kero kubwa kwa wanaotumia barabara hiyo kila wakati kwenda kwenye
shughuli zao za kila siku.

Hali halisi ndio hivi mvua ikinyesha jijini Dar,kwa eneo la Bamaga.

Maji yakiwa yametuama tuliiii eneo la bamaga kuelekea Afrikasana.
Sehemu
ya soko la Mboga mboga na Matunda la Afrikasana-Sinza likiwa
limezungukwa na maji,hali iliyopelekea biashara kuwa ngumu eneo hilo.
