Michuano ya kuogelea ya Kanda ya 4
Afrika imemalizika mjini Luanda, Angola huku Afrika ya Kusini ikiibuka
kidedea. Nchi nyingine zilizoshiriki ni Mauritius, Msumbiji, Botswana,
Uganda, Kenya, Tanzania na wenyeji Angola
Zaidi ya washiriki 2,00o
walishindana katika aina mbalimbali (categories) za mashindano hayo
kama vile michezo ya butterfly mita 200, free style ya mita 100 na mita
200 kwa mchezaji mmoja mmoja (individual).Habari kutoka Luanda zinasema katika matokeo ya ujumla kwa upande wa wanaume, Afrika ya Kusini imeongoza, ikifuatiwa na Angola, Kenya, Botswana, Zambia, Msumbiji, Uganda, Mauritius na Tanzania ikiwa ya mwisho
Kwa upande wa wanawake, Afrika ya Kusini iliongoza, ikifuatiwa na Zambia, Angola,Mauritius,Kenya, Msumbiji,Botswana, Tanzania na Uganda
Katibu Mkuu wa chama cha kuogelea nchini Tanzania (TSA), Noel Kiunsi alikuwa na mategemeo ya timu yake kufanya vizuri lakini mambo yamekwenda tofauti.
