.jpg)
Waziri
wa Elimu na Mafunzo Dkt Shukuru Kawambwa akielezea Jambo katika Mkutano
kati ya viongozi wa elimu kutoka wa Tanzania na Viongozi wa Wizara ya
Elimu ya nchini Singapore.
.jpg)
Viongozi
wa Wizara ya Elimu na Mafunzo kutoka Tanzania na Viongozi wa Elimu wa
Singapore wakiwa katika mkutano wa pamoja katika kubadilisha mbinu na
mikakati mbalimbali ambayo inaweza kuboresha na kuleta mageuzi katika
mifumo ya elimu wa nchi hizi mbili.
.jpg)
Waziri
wa Elimu na ujumbe wake wakiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa
Chuo kikuu cha Taifa Singapore. Ujumbe wa Tanzania ulitembelea chuo
hicho ili kujionea na kujifunza ambavyo elimu ya ngazi ya chuo kikuu
inavyotolewa nchini Singapore.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa
pamoja na viongozi wa elimu nchini wametembelea Singapore kujifunza jinsi nchi
hiyo ilivyofanya mageuzi makubwa katika mfumo wa elimu na mafunzo.
Mfumo wa elimu wa nchi hiyo, unalenga kuendeleza wanafunzi katika
kuwapatia stadi muhimu zinazohitajika kwa maendeleo ya nchi.
Mfumo wa elimu wa nchi hiyo, umeweka mkazo zaidi katika kutoa mafunzo ya
ufundi stadi ambayo yanatoa ujuzi kwa mhitimu kuweza kufanya kazi katika
kada ya kati. Takwimu za elimu zinaonyesha kuwa, asilimia 29.4 ya wahitimu
wanajiunga na vyuo vikuu; asilimia 28.2 wanajiunga na vyuo vya elimu ya
ufndi na asilimia 46.4 wanajiunga na vyuo vya utaalamu mbalimbali
(Polytechnic).
Katika ziara hiyo Dkt Kawambwa na ujumbe wake walipata nafasi ya
kutembelea chuo kikuu cha Taifa cha Singapore (National University of
Singapore), Chuo cha Elimu ya Ufundi (Institute of Technical Education) na
Chuo cha Ufundi stadi (Republic Polytechnic) ambapo katika vyuo hivyo
walipata nafasi ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi
pamoja na walimu.
na michuzi media