Wastara, akiwa katika gari lililokuwa likiendeshwa na msanii mwenzake, Bond Bin Suleiman majira ya saa nne usiku maeneo ya Tabata, walipata ajali hiyo baada ya gari lisilofahamika, kukatiza kabla mbele yao na dereva alipofunga breki ghafla, muigizaji huyo ambaye hakuwa amevaa mkanda wakati huo, alitoka kwenye kiti na kwenda kujigonga kwa nguvu kwenye ‘dashboard’.
Kitendo hicho cha kujigonga kwa nguvu kilisababisha kujichana sehemu ya juu ya jicho lake la kulia, kitu ambacho kilimpa maumivu makali. Alipokwenda kupata matibabu katika zahanati ya Kilimanjaro, alihudumiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
“Si bure, kutakuwa na kitu tu kisicho cha kawaida kwangu, lakini naamini Mungu yupo upande wangu, maana ajali hizi zote ni mbaya ambazo ningeweza kabisa kupoteza uhai,” alisema muigizaji
huyo.
GPL