Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia Prof Makame Mbarawa.
Serikali
imesema jumla ya watanzania milioni 12.3 wanaakaunti za kutuma na
kupokea pesa kwa kutumia mitandao mbalimbali ya simu nchini.
Prof. Mbarawa amesema kwa kutumia mfumo huo zaidi ya shilingi trilioni 28.3 zimetumwa na wateja wa mitandao hiyo kupitia huduma za simu za mkono.
Ameongeza kuwa makampuni hayo ya simu pia yametoa ajira kwa watu laki mbili pamoja na ajira milioni 1.5 sizizo za moja kwa moja.
chanzo: EATV.TV